Uongozi wa vikosi vya usalama nchini Kenya maarufu kama KDF umempandisha cheo koplo Joyciline Jepkosgei hadi cheo cha usajenti kutokana na ufanisi wake katika mashindano ya London Marathon ambako alimaliza katika nafasi ya pili.
Sherehe hiyo imefanyika katika makao makuu ya KDF ikiongozwa na mkuu wa majeshi Robert Kibochi lakini pia kiongozi wa masuala ya michezo kwenye vikosi vya usalama Kanali Benjamin Kiprop pamoja na viongozi wengine ambao wamehudhuria sherehe hiyo.
Jepkosgei ambaye alikuwa anatetea ubingwa wake alimaliza nafasi ya pili baada ya musa wa masaa 2;18;07 nyuma na muethiopia Yalemzerf Yehualaw aliyemaliza wa kwanza kwa muda wa masaa 2;17;43.
Jepkosgei mwenye umri 28 alijitambulisha kwenye dunia ya riadha kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2019 aliposhinda mbio za marathon za New York Marekani.

