WABUNGE KAUNTI YA TAITA TAVETA WAWEKA MIKAKATI YA KUWASILISHA MISUADA KATIKA BUNGE LA KITAIFA.

Wabunge wa Kaunti ya Taita taveta sasa wanajiandaa kuwasilisha miswaada bungeni itakayosaidia wakazi wa kaunti hiyo kunufaika kutokana na raslimali ya mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Tsavo kufuatia utata unaoshuhudiwa kwa sasa.

Wakiongozwa na mbunge wa Taveta John bwire, Wanasema wakaazi wameathiriwa pakubwa na wanyamapori wala hakuna fidia wanayopewa na shirika la huduma kwa wanyamapori KWS licha ya baadhi yao kupoteza maisha Yao huku wengine wakijeruhiwa vikali.

Ni Kauli iliyoungwa mkono na spika wa bunge la kaunti ya Taita tavet Wisdom Mwamburi, akiahidi kushirikiana na wawakilishi wadi kuunda sheria zitakazotoa suluhu mwafaka na ya kudumu.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya maandamano ya kudai haki ya wawakilishi wadi katikaa Afisi kuu ya kws mjini Voi kutibuka,baada ya waandamanaji kurushiwa vitoa machozi na maafisa wa polisi