AFUENI KWA WAFANYABIASHARA YA MIFUGO KAUNTI YA LAMU.

Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdallah Timmamy amesema kuwa wafugaji katika kaunti hiyo na kaunti jirani, watanufaika hata zaidi kwani taifa la Oman linanuia kununua mifugo na kuwasafirisha hadi nchini humo, kupitia bandari ya Lamu.

Timammy amesema hatua hiyo itanufaisha kaunti ya Lamu kiuchumi kupitia mapato ya bandari hiyo ya Lappset, mbali na kuwa itawanufaisha wakaazi wanaojishughulisha na ufugaji.

Balozi wa Oman Sheikh Swaleh Al arith, pamoja na Timammy wamezuru mashamba ambayo yatahifadhiwa mifugo hao kabla ya kusafirishwa.

Gavana Timammy amesema kuwa meli ya kwanza ya kusafirsha mifugo hao inatarajiwa kuwasili Lamu hivi karibuni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *