UTUMIZI WA DAWA ZA KULEVYA KUPITIA SINDANO WAWAWEKA VIJANA KATIKA HATARI YA KUPATA UKIMWI.

Asilimia 18.7 ya vijana wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano, wametajwa kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi kaunti ya Kwale.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la kijamii la kukabiliana na utumizi wa mihadarati kaunti ya KWALE, la Teenswatch Ahmed Mohammed anayetaka hamasa zaidi kutolewa kwa vijana ili kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.

Kulingana na Mohammed, maambukizi miongoni mwa vijana, ni ya kutamausha kufuatia utafiti wa baraza la kitaifa, la kupambana na Ukimwi (NSDCC), unaonyesha kuwa asilimia 3.2 ya wakaazi wa Kwale wanaishi na VIRUSI vya ukimwi.

Kwa upande wake mshauri wa maswala ya kiafya kutoka baraza la kitaifa la vijana (NYCC) Rose Otaye, amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Otaye amesema kuwa tayari mashirika mbali mbali nchini, yamepokea msaada wa kifedha ili kupunguza maambukizi hayo miongoni mwa waraibu.