Afisa wa kurekebisha tabia za watoto kwenye mahakama ya Mpeketoni kaunti ya Lamu Dhashrifa Mohammed, amesema wazazi wengi wametelekeza majukumu yao ya ulezi.
Hii ni baada ya kukithiri kwa visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa watoto wenye umri mdogo, hali inayotajwa kusababishwa na malezi duni kutoka kwa wazazi wa watoto hao.
Dhashrifa amewataka wazazi kujukumika katika malezi ya wanao, sawia na kudumisha ushauri nasaha mara kwa mara, kwa watoto hao ili kuhakikisha kuwa kuna unyoofu wa maadili.

