Mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate, amekitaka kikosi chake kuonyesha uwezo na kiwango zaidi kwenye mechi na mashindano yajayo.
Kocha Southgate amesema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mataifa Ulaya dhidi ya Ujerumani mchezo utakaochezwa siku ya leo.
Uingereza walishuka daraja kwenye mechi za Ligi ya Mataifa Ulaya kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Italia jambo ambalo kocha huyo amekiri kukerwa nalo kiasi cha kuwataka wachezaji kuimarika zaidi kiuchezaji.
Kwa sasa Uingereza hawatakuwa na mchezo mwingine wa nje baada ya huo wa Ujerumani mpaka pale watakaposafiri kwenda Qatar kwa mashindano ya kombe la dunia.

