Aliyekuwa mwakilishi wa wadi mteule wa Shella kaunti ya Lamu baada ya kushinda kwenye kipute hicho katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu wa 2022 Azhar Ali Mbarak amechaguliwa kuwa spika wa bunge la kaunti ya Lamu.
Mbarak alikuwa amechaguliwa kama mwakilishi wa wadi mteule wa Shella kabla ya kujiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita na kujitosa kwenye kipute hicho cha kuwania nafasi ya Uspika katika bunge la kaunti hiyo.
Katika taarifa yake amewataka wawakilishi wa wadi kwenye kaunti ya Lamu kushirikiana ili kufanikisha maendeleo kwa wenyeji na kuwataka kuweka kando tofauti zao za kisiasa.
Aidha, amesema ni wakati wa viongozi kufanya kazi ipasavyo kwa mujibu wa katiba ili kuhakikisha wanafanikisha ahadi ambazo walizitoa kwa wenyeji wa kaunti ya Lamu.

