UEFA YAIPIGA URUSI MARUFUKU

Kamati kuu ya Uefa imeitoa Urusi katika orodha ya timu za taifa zitakazo shiriki katika mechi za kufuzu kwa mashindano ya UERO mwaka 2024 taarifa ambayo imethibitishwa na shirikisho la soka la Urusi baada ya kikao cha jana cha kamati hiyo.

Timu ya taifa ya Urusi pamoja na vilabu vyote vya nchi hiyo vilipigwa marufuku na kamati ya UEFA kutoshriki mechi yoyote ya kimataifa mwezi February mwaka huu kutokana na taifa hilo kuivamia Ukraine na kusababisha uharibifu wa mali pamoja na kupoteza maisha ya wananchi.

Urusi sasa haitashiriki hata mashindano ya kombe la dunia yaliyoratibiwa kufanyika mwisho wa mwaka huu nchini Qatar pamoja na mashidnano ya Euro ya wanawake yaliyofaa kufanyika Uingereza na nafasi yao kuchukuliwa na ureno.

Wizara ya mambo ya ndani ya taifa la Ujerumani imeomba kamati ya UEFA kupiga marufuku Belarus kwa kushirikiana na Urusi kuivamia Ukraine.