Zaidi ya punda 5 hufariki kila wiki mjini Lamu kwa sababu ya ukosefu wa lishe bora.
Haya ni kwa mujibu wa daktari wa punda kaunti hiyo Obadiah Singoi ambae amesema ukosefu wa lishe hulazimu mifugo hao kula plastiki ambazo husababisha uvimbe kwenye tumbo la mnyama huyo na kuzuia usagaji wa chakula.
Kwa upande wake mkurugenzi wa maswala ya mifugo mjini Lamu Jamila Mitsanze ametoa wito kwa wakaazi kuhakikisha haki za wanyama hao hazihujumiwi

