NICK MWENDWA AREJEA KATIKA OFISI YAKE YA KANDANDA HOUSE

Rais wa shirikisho la soka la FKF Nick Mwendwa ambaye amerejea katika ofisi yake ya Kandanda House iliyoko Kasarani, kaunti ya Nairobi baada ya kufungwa kwa ofisi hizo kwa kipindi cha miezi 11.

Amesema kuwa kwa sasa wanalenga kufanya mikutano na viongozi wa vilabu vya soka nchini Kenya kwenye mazungumzo ambayo yatasaidia taifa hili kuondolewa marufuku ya kutoshiriki mechi za kimataifa na Fifa.

Mwendwa aliyekuwa ameandamana na wanahabari, maafisa wa polisi pamoja na viongozi wengine wa FKF akiwemo mkurugenzi mkuu wa Barry Otieno ameeeleza matumaini yake marufuku hiyo itaondolewa katika siku chache zijazo.

Aidha Mwendwa ameeleza furaha yake ya kuona kwamba harakati za kuanza kukomboa soka la Kenya zimeannza rasmi kwani hatua ya kwanza ilikuwa kurudishwa kwa fkf iliyodhabiti kisha mazungumzo kuanza rasmi na shirikisho la kimataifa FIFA.

Hata hivyo amemshukuru rais wa taifa hili Wiliam Ruto kwa kulipa shirikisho hilo mazingira mazuri ya kufanya kazi ya kurudisha hali shwari kwenye soka la Kenya.