Seneta wa kaunti ya Mombasa Mohammed Faki, ameahidi kutekeleza maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo, kupitia kwa serikali ya kaunti.
Kulingana na Faki atahakikisha serikali ya kaunti ya Mombasa, inazingatia sheria za utekelezwaji wa maendeleo kwa wananchi kwa mujibu wa katiba.
Akizungumza katika kaunti hiyo, Faki amewataka wananchi kutohofia suala lolote katika masuala ya uongozi wa kaunti ya Mombasa.
Vilevile amewaonya wananchi dhidi ya kuwa na dhana potofu, kuhusiana na Maseneta kuwa vibaraka wa magavana katika serikali za kaunti na hata kushirikiana katika ufujaji wa fedha za umma.

