Spika anayeondoka mamlakani katika bunge la Kaunti ya Kilifi Jimmy Kahindi, amewashauri wale wanaotaka kuwania wadhifa huo kuhakikisha kuwa wako tayari, kukabiliana na changamoto zinazo andamana na majukumu ya wadhifa huo.
Haya yanajiri siku chache baada ya kiongozi huyo kuweka wazi kuwa hatawania wadhifa huo kwa awamu ya tatu, tangu ujio wa serikali za kaunti humu nchini.
Kahindi amewataka wagombea wa wadhifa huo kuendeleza kampeni zao kwa njia ya sawa na uwazi na kupuuzia uvumi kuwa anapania kuwania tena uspika wa bunge la kaunti ya Kilifi.
Aidha, amewataka viongozi waliochaguliwa katika bunge hilo pamoja na wafanyakazi wa bunge la Kaunti, kushirikiana na spika mpya atakae ingia katika nafasi hiyo.
JIMMY KAHINDI AWASHAURI WANOTAKA KUWANIA WADHIFA WA USPIKA KWENYE BUNGE LA KAUNTI YA KILIFI KUJIANDAA

