WILLIAM SAMOEI KIPCHIRCHIR ARAP RUTO AMEAPISHWA KUWA RAIS WA TANO WA KENYA

Sasa ni rasmi kuwa rais wa tano wa Kenya ni William Samoei Kipchirchir Arap Ruto.

Rais Ruto atakuwa rais wa tano wa Kenya baada ya kuapishwa rasmi mbele ya umma kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Rais Ruto amekabidhiwa zana za  utawala ambazo ni nakala ya katiba ya sasa na kitara cha kijeshi na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama ishara ya mamlaka ya kuliongoza taifa la Kenya.

Viongozi na ujumbe mbalimbali kutoka mataifa barani afrika wamehudhuria na kushuhudia uapisho wa rais William Ruto.

Viongozi hao wamejumuisha marais akiwemo rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, rais wa Komoro, Azalia Sumi, rais wa jamhuri ya Demokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, Rais wa Brazaville Dennis Asongozo, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, rais wa Malawi, Lazurus Chakwera, rais wa Rwanda Paul Kagame, rais wa Somalia, Hassan sheikh Mahamoud, rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embaló, Rais wa msumbiji Filipe Nyusi, Salva Kiir wa sudani kusini, rais wa Zimbambwe Emmerson Mnangagwa, waziri mkuu wa Ethiopia Abbey Ahmed miongoni mwa viongozi wengine.