WAZAZI WALAUMIWA KWA KUTELEKEZA MAJUKUMU YAO YA ULEZI.

Gavana wa kaunti ya Mombasa, Abdulswamaad Shariff Nassir amewaonywa vijana dhidi ya kusingizia ukosefu wa ajira, kuwa chama cha wao kujihusisha na uhalifu kwenye jamii.

Kulingana na gavana huyo, vijana wote wanao jihusisha na masuala ya uhalifu, wanapaswa kuwa wakiendeleza masomo na hivyo kusema kuwa huenda ikawa baadhi ya wazazi, wamelegea katika kufanikisha wajibu wao wa malezi kwa wanao.

Akizungumza na waandishi wa habari, gavana Nassir amesema kuwa kuna haja ya wazazi, kushirikiana na viongozi wa kidini, ili kuwapeleka wanao katika shule zilizo chini ya nyumba za ibada, kwani huenda wakasaidika kupata mwelekeo wa maisha.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na viongozi wa dini hiyo kaunti ya Mombasa, wakiongozwa na Mohammed Salimu, ambao wamewaonya vijana wa kiislamu dhidi ya kukiuka sheria za dini hiyo huku Mwanasiasa Said Abdullah, akipongeza juhudi za kuboresha usalama wa kaunti hiyo.