Jamii kaunti ya Kilifi imeonywa dhidi ya kuwalaumu viongozi wa kisiasa, kutokana na kucheleweshwa kwa miradi ya maendeleo mashinani.
Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi wadi ya Mnarani kaunti ya Kilifi, Juma Chengo ambaye amesema kuwa hatua hiyo, inatokana na kucheleweshwa kwa magao wa fedha za serikali ya kaunti na wala sio wawakilishi wadi.
Juma ameelezea kuwa, wanakandarasi wengi wamekuwa wakikosa kukamilisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi waliokabidhiwa na serikali ya kaunti ya Kilifi, kutokana na kucheleshwa kwa malipo yao, kwa mujibu wa makubaliano kati yao na serikali ya kaunti ya Kilifi.
Ameongeza kuwa, kucheleweshwa kwa fedha za maendeleo na basari, pia kumeathiri shughuli za masomo ya wanafunzi kwenye jamii wadi yake, licha ya idadi kubwa ya wale walionufaika na ufadhili huo, kuwa wanafunzi wa jinsia ya kike.

