VYUO VIKUU NCHINI VYATAKIWA KUSHIRIKIANA NA MATAIFA YA KIGENI ILI KUBORESHA SHUGHULI ZA MASOMO.

Katibu wa Elimu ya Juu na Utafiti kwenye wizara ya elimu nchini Dkt. Beatrice Inyangala, amekipongeza Chuo Kikuu cha Taita Taveta, kwa ubora wake wa kitaaluma na ushirikiano na mataifa ya kigeni.

Kulingana na katibu huyo, kuna haja ya vyuo vikuu nchini kutambua changamoto zake na kushirikisha wizara hiyo, katika kutafuta wafadhili wa kuwasaidia kukabiliana na changamoto hizo.

Akizungumza baada ya kuzuru chuo, katibu Inyangala amesema kuwa ushirikiano kati ya shirika la ujerumani la DAAD na chuo hicho cha Taita Taveta, umesaidia pakubwa kupandisha hadhi ya masomo ya chuo hicho.

Kwa upande wake Naibu Chansela wa chuo hicho Fred Simiyu, ameelezea kuwepo kwa mipango mingi ya ushirikiano kati ya chuo hicho na shirika hilo la Ujerumani la DAAD.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *