Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, imeelezea utayari wake katika kufanikisha shughuli za uchaguzi mdogo, wa nafasi mbali mbali za uongozi katika taifa hili.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa tume hiyo Marjan Hussein Marajan, wamelazimika kuharakisha mikakati hiyo, ili kuwapatia makamishna wapya watakao chaguliwa wakati rahisi wa kutekeleza zoezi hilo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Marjan amesema kuwa chaguzi hizo ndogo, zinatarajiwa kufanyika katika maeneo bunge tatu kote nchini na wadi 13 kitaifa.
Kulingana na Marjan, huenda idadi hiyo ikaongezeka, kutokana na kesi ambazo bado zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbali mbali za taifa hili.
Ikumbukwe kwamba eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, ni mojawapo ya maeneo ambapo wananchi, wanatarajiwa kushiriki shughuli za uchaguzi mkuu.

