Uteuzi wa wawakilishi wa wadi wateule wa chama cha ODM kwenye bunge la kaunti ya Mombasa unaendelea kuibia hisia mseto kwa baadhi ya wale ambao majina yao yalikosekana kwenye orodha ya waliopaswa kuteuliwa.
Kulinagana na Victor Wesonga anasema ametamaushwa na hatua ya baadhi ya majina kukosekana na kisha nafasi hizo kupewa watu wengine kutoka kaunti zingine.
Wesonga anasema kuna baadhi ya watu walioweka juhudi kwa chama cha ODM kwa miaka mingi ili kizidi kuwa na umaarufu ila wakati wa uteuzi hawakabidhiwi nafasi hizo.
Amelalamikia unyanyasaji katika chama hicho na kumtaka kianara wa chama hicho Raila Odinga kuingilia katika ili kupatikane mwafaka.

