SERIKALI YAPANIA KUJENGA MAKAVAZI KATIKA MSITU WA SHAKAHOLA KAUNTI YA KILIFI.

Huenda serikali ya kitaifa ikajenga makavazi katika eneo la Shakahola ili kuwapa wakenya kumbukumbu ya vifo vya wakenya zaidi ya 100 katika eneo hilo kutokana na masuala ya itikadi kali.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani nchini Kithure Kindiki ambaye amesema kuwa bado serikali inaendelea kujadiliana kuhusiana na mwelekeo ambao serikali itachukua shamba hilo linalo daiwa kuwa la ekari mia nane.

Waziri huyo amesema kuwa serikali itatoa tangazo ramsi la kujengwa kwa makavazi hayo katika eneo hilo, pindi shughuli za ufukuzi wa miili pamoja na uchunguzi wa chanzo cha vifo hivyo waumini wa kanisa la Good News International linalo ongozwa na mchungaji tata Paul Mackenzie utakapo kamilika.

Aidha Waziri huyo pia amewapongeza wanahabari kwa kuwa katika mstari wa mbele katika kupeperusha taarifa za awali kuhusiana na mauaji ya halaiki katika eneo hilo la Shakahola licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo suala la wao kuzuiliwa kuingia ndani yam situ huo.