Hatua ya serikali za kaunti kutoa ufadhili wa karo kwa wanafunzi ni njia mojawapo ya kuwasaidia wazazi, kufanikisha majukumu yao ya kuwasomesha wanao.
Haya ni kwa mujibu wa mwanasheria mkuu kaunti ya Kwale, Salim Gombeni ambaye ametetea mpango wa serikali za kaunti kutoa ufadhili wa basari kwa wanafunzi, akisema kuwa mpango huo haupaswi kusitishwa.
Akizungumza katika kaunti hiyo, Gombeni amesema kuwa wazazi wengi husaidiwa na serikali za kaunti kugharamikia elimu ya wanao, kutokana na changamoto za kiuchumi kwenye jamii.
Aidha, ameongeza kuwa ugavi wa fedha za basari kwenye serikali za kaunti, umekuwa ukizingatia sheria za kaunti pamoja na zile za kitaifa.

