SEKTA YA UTALII KAUNTI YA KILIFI YATARAJIWA KUBOREKA.

Serikali ya Italia inaendeleza juhudi za kufufua sekta ya utalii katika kaunti ya kilifi, kwa kuhakikisha kuwa watalii zaidi wanazuru kaunti hii.

Akizungumza katika eneo la Gede Ruins, kwenye tamasha la kitamaduni la muziki wa kitaliano, balozi wa Italia humu nchini Roberto Natali, amesema kuwa mpango huo ni sehemu ya kujenga uhusiano bora zaidi, kati ya taifa hilo na Kenya.

Natali amekariri kuwa, tamasha hilo linalenga kuvutia watalii zaidi kutoka taifa la Italia hadi Kenya na hususan kaunti hii ya kilifi, ili kushuhudia tamaduni zao.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro amesema kuwa serikali yake, imeweka mikakati zaidi ya kufufua sekta ya utalii katika eneo la Malindi na Watamu.

Wakati huo huo Mbunge wa Kilifi kaskazini, Owen Baya  amemshukuru balozi wa Italia, kwa kuandaa tamasha hilo huku akisistiza haja ya maeneo zaidi ya kitalii eneo hilo, kuangaziwa ili kuvutia watalii kwa wingi.