Naibu spika wa bunge la kaunti ya Tana River Rhoda Katisha ametaja ushindi wake kwenye wadhifa huo kama ushindi kwa wanawake wote.
Amesema ushindi wake ni historia katika kaunti hiyo kwani tangu kuanzishwa kwa ugatuzi nchini hakujawahi kuwa na naibu spika wa kike katika bunge la kaunti hiyo.
Katisha ambaye ni mwakilishi wa wadi ya Garseni amewataka wanawake kujitokeza na kuwania nafasi za uongozi nchini.
Vilevile, amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kwa wanawake katika kuwania nafasi za uongozi nchini ni vyema iwapo wataweka kujihusisha kiukamilifu kwenye nafasi za uongozi.

