RAIS WILLIAM SAMOEI RUTO AMWAGIZA WAZIRI WA KITHURE KINDIKI KUIMARISHA USALAMA

illiam Ruto amemwagiza waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki kuimarisha usalama katikati mwa jiji la Nairobi ambapo wanasiasa wa Azimio wanapanga kufanyaa maandamano kulalamikia kuwang’atuliwa ofisini kwa makamishna watatu wa IEBC.
Rais Ruto akisema ni haki kwa upinzani kuandamana, japo akaonya kuhusu uharibifu wa mali.
Ni kauli iliyoungwa mkono na naibu rais Rigathi Gachagua ambaye amewaonya wanaazimio kutotatiza shughuli za kiuchumi katika maandamano hayo.
Aidha viongozi hao wamemkosoa Raila Odinga wakisema hatua na harakati alizoanzisha kwa sasa ni njama ya kulazimisha handsheki nyingine na serikali ya sasa.
Hatahivyo viongozi hao wa Kenya kwanza wamesema kuwa maandamano hayo yasichangie kuzorotesha uchumi ambao tayari uko katika hali mbaya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *