RAILA ODINGA AWEKA WAZI MAPUNGUFU YA SERIKALI YA KWENYE KWANZA.

Viongozi wa chama cha ODM, wanaendeleza maadhimisho ya miaka 20 tangia chama hicho kilipo anzishwa.

Maadhimisho hayo ambayo yanaendelea katika kaunti ya Busia, yanatarajiwa kuweleta pamoja viongozi mbali mbali wa chama hicho na pamoja na wafuasi wao wanaotaka kufahamu uamuzi wa aliyekuwa kinara wa chama hicho Raila Odinga, baada ya kukosa kuchanguliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya muunagano wa mataifa ya Afrika AUC.

Akizungumza mda mfupi uliopita katika kikao na waandishi wa habari, Odinga ameishtumu serikali kwa kuendeleza kampeni za wakenya kusajiliwa kwenye SHA na kutaka changamoti zinazo kumba bima hiyo kutatuliwa.

Vile vile Raila ametoa wito wa kusitishwa kwa visa vya wakenya kutekwa nyara na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa polisi na kisha baadae kupatika wakiwa wameaga dunia.