NANCY MACHARIA AKAMILISHA MDA MWAKE WA KUHUDUMU KATIKA WADHIFA WA MKURUGENZI WA TUME YA WALIMU TSC.

Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, imeanza mchakato wa kumtafuta afisa mkuu mtendaji mpya, atakayemrithi Nancy Macharia, ambaye muda wake wa kuhudumu unakaribia kukamilika.

Macharia, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza tume hiyo tangu ibuniwe, amekuwa amekuwa akihudumu katika wadhifa huo tangu mwaka 2015.

TSC iweka tangazo rasmi la uteuzi wa mrithi wa Macharia na kuwataka waliohitimu kutuma maombi.

Afisa mkuu mtendaji wa TSC, huwa na anahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, ambacho huongezwa mara moja.