Mwenyekiti wa bandari ya LAPSSET, Ali Mbogo amelalamikia uharibifu wa fedha za umma ambazo hutokana na ushuru, unaokusanywa na serikali ya kaunti ya Mombasa.
Mbogo amedai kuwa kaunti ya Mombasa, hukusanya ushuru mkubwa zaidi na pia, hupokea mgao mkubwa sana kutoka kwa hazina ya kitaifa, ila hakuna maendeleo ambayo yameshuhudiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mbogo amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 13, tangia kuanzishwa kwa serikali za ugatuzi nchini, bado wakaazi wa kaunti hiyo wameendelea kushuhudia changamoto mbali mbali za kijamii.
Mbogo amedai kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa, imezingatia pakubwa masuala ya mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wake na wala sio kuyapatia kupaumbele, matatizo ya wakaazi wa kaunti hiyo.