MUUNGANO WA WANAHABARI UMEANZISHA MRADI WA KUHAMASISHA WAANDISHI WA HABARI

Muungano wa wanahabari nchini Kenya Correspondents Association(KCA), umeanzisha mradi wa kuhamasisha waandishi wa Habari katika kaunti mbalimbali nchini, kuhusu jinsi yakukabiliana na Habari gushi hususan zinazoenezwa mitandaoni.
Hatua hii inajiri baada ya ripoti iliyotolewa na shirika linaloshughulikia wanahabari kifungu 19, kuonyesha kuwa asilimia 75 ya wakenya hawawezi kubainisha iwapo, Habari ni sahihi ama ni ghushi.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Mkurugenzi wa shirika la Ujamaa Center mjini Mombasa, Patric Ochieng amesema kuwa jambo hilo limeathiri jamii kwa kiwango kikubwa, hasa katika kufanya maamuzi.
Wakati uohuo,mwenyekiti wa shirika la KCA William Oloo Janak, amesema kuwa mradi huo utawawezesha waandishi wa Habari, kubainisha Habari sahihi na gushi ambazo, zimewanyima wananchi uhuru wa kuafikia Habari sahihi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *