Mwenyekiti wa Muungano wa wanahabari nchini Kenya Correspondents Association(KCA), William Oloo Janak ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana na waandishi wa habari ili kupata taarifa kwa urahisi kwenye taasisi za Kiserikali ili kuwajuza kiukamilifu wananchi yanayojiri nchini.
Akizungumza kwenye kongamano la waandishi wa habari mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, Oloo amesema wanahabri mbalimbali kanda ya pwani wamekuwa wakilalamikia changamoto ya kutopata taarifa hizo kutoka kwa idara mbalimbali.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Baya Kitsao ambaye ni mshirikishi wa muungano huo ambaye amesema hali hiyo imeathiri kwa kiwango kikubwa utendakazi wa wanahabari kanda ya pwani na chini kote.
KCA YATOA WITO KWA WADAU MBALIMBALI KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI WA HABARI
