Waziri wa leba nchini Florence Bore amesema jumla ya watahiniwa 32,276 wanashiriki mtihani wa kitaifa wa taaluma mbalimbali kwenye Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Viwanda ( NITA) na wanafunzi 500 wakiwa ni wa kutoka kanda ya pwani.
Katika taarifa yake kwa wanahabari akiwa kaunti ya Mombasa amesema idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 45.2 ikilinganishwa na watahiniwa ambao walishiriki mtihani huo mwezi Agosti mwaka huu wa 2022.
Amesema mitihani hiyo pia inaendelea katika taasisi zingine za mafunzo ya kiufundi za kiserikali nchini.
Amewahimiza wanafunzi wanaonufaika na taasisi hizo kutumia ujuzi wanaopata ili kujiendeleza kimaisha.
Florence Bore amesema kuna uhaba wa taasisi hizo nchini na kuahidi serikali itaweka mikakati kuhakikisha kunajengwa zingine ili kuboresha sekta ya elimu katika taifa hili, kauli ambayo imeungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa NITA kaunti ya Mombasa Stephen Ogenga.
JUMLA YA WATAHINIWA 32,276 WANASHIRIKI MTIHANI WA KITAIFA WA TAALUMA MBALIMBALI KWENYE MAMLAKA YA NITA
