Baadhi ya viongozi wa kisiasa kaunti ya Mombasa wamejitokea kukashifu vikali mauaji ya afisa mkuu wa IEBC kaunti ya Kilifi Aisha Akinyi Abubakar.
Wakiongozwa na seneta wa kaunti ya Mombasa Mohamed Fakii na mbunge wa Kisauni Rashid Benzimba, wamesema kuwa sharti uchunguzi wa haraka dhidi ya mauaji hayo ufanyike.
Wakizungumza na wanahabari, viongozi hao wamesisitiza haja ya wahusika wa mauaji hayo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na mwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa, Zamzam Mohamed, ambaye amekisia kuwepo kwa mipango ya kufanikisha mauaji hayo.
Afisa huyo alikumbana na kifo hicho mnamo jumapili asubuhi saa tisa, baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi waliokuwa wamejihami kwa vifaa butu.

