Kinara wa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga anapotarajiwa kuongoza maandamano siku ya Jumatano wiki hii ili kupinga kuondolewa ofisini kwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, hisia mbalimbali zinaendelea kutolewa kuhusiana na suala hilo.
Akitoa hisia zake mkereketwa wa masuala ya kisiasa katika eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi Japhet Ria amewataka wenyeji kusitisha maandalizi ya maaandamano kupinga kuondolewa ofisini kwa makamishna hao wanne.
Kwa kujibu wa Mkereketwa huyo kipindi cha siasa kilikamilika na sasa wananchi wanapaswa kuwapa nafasi viongozi waliochaguliwa ili kutekeleza ahadi ambazo walizitoa wakati wa kampeni zao za uchaguzi.
Ria ambaye alikuwa akizungumza akiwa Kaloleni amesema iwapo maandamano hayo yatafanyika huenda yakachagia kusambaratika kwa uchumi wa nchi.
Vilevile, ameunga mkono harakati za bunge la kitaifa wa kutimuliwa afisini makamishana wanne wa IEBC akidai walikiuka katiba ya nchi kutokana na kile ambacho anasema walipania kulifanya taifa hili kutumbukia katika ghasia za baada ya uchaguzi kama mwaka 2007 na 2008.
HISIA MSETO ZINAENDELEA KUTOLEWA KUHUSU MAANDAMANO YA MUUNGANO WA AZIMIO
