GAVANA MUNG’ARO AWAKOSOA BAADHI YA VIONGOZI WA KAUNTI YA KILIFI

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mung’aro amewakosoa baadhi ya viongozi wa kaunti hii ambao wamekuwa wakipinga mpango wa kuwafadhili wanafunzi kimasomo hasa wale ambao wanasomea kwenye shule za kitaifa kwenye kaunti zingine licha ya kutoka hapa Kilifi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari akiwa eneo la Tezo, Gavana Mung’aro amesema viongozi ambao wanapinga mpango huo ni wale ambao hawajali elimu ya watoto wa kaunti hii ya Kilifi .
Amesema ataendeleza juhudi zaidi na kuhakikisha wanafunzi wa kaunti ya Kilifi wanasoma bila kukabiliwa na changamoto zozote ili kuafikia ndoto zao za maisha.
Aidha, amesema wizara ya elimu imetayarisha hundi za watoto zaidi ya elfu 2 ili kuwalipia karo wanafunzi hao kwenye muhula wao wa pili shuleni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *