Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, ameibua madai ya kushurutishwa ajiuzulu na hata kuahidiwa shilingi bilioni bilioni mbili.
Kulingana na Gachangwa, hatau yake kubanduliwa kwenye wadhifa wa naibu wa rais katika taifa hili, hauku zingatia sheria na ulichangiwa pakubwa na misimamo yake anayodai ilikuwa mikali dhidi ya serikali kuu.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari, Gachagwa ameelezea kuwa sio lazima ahudumu kwenye nyadhifa kuu serikalini, kwa kile anachosema kuwa hana taamaa ya uongozi.
Wakati uo huo Gachagwa, amewakosoa viongozi wa bunge la kitaifa nchini, kutokana na hatua ya viongozi hao kutokuwa na msimamo thabiti dhidi ya ajenda za serikali ya Kenya kwanza.

