BELIO KIPSANG AWATAKA WALIMU KUJIANDAA KUANZA MASOMO YA NGAZI YA CHINI

Huku kongamano la walimu likiingia siku yake ya tatu leo Jumatano kwenye kaunti ya Mombasa, wadau wa sekta ya elimu wamekubaliana na agizo la rais William Samoei Ruto kuwa wanafunzi wa ngazi ya chini ya sekondari wasalie katika shule za msingi.
Akimwakilisha Rais Ruto kwenye kongamano hilo, katibu katika wizara ya elimu nchini Belio Kipsang amewataka walimu kujindaa kuanza masomo ya ngazi ya chini ya sekondari mwezi ujao wa Januari.
Kipsang amesema kuna uwezekano kuwa shule zinazokaribiana zitahitaji kutumia kwa pamoja maabara huku serikali ikijitahidi kujenga maabara katika shule za msingi.
Aidha Kipsang amesema ufadhili wa serikali utaimarishwa na kusalia kwa wanafunzi wa ngazi ya chini ya Sekondari (Junior Secondary) kwenye shule za msingi kutasaidia kwa kiwango kikubwa katika kufanikisha asilimia 100 ya wanafunzi ambao wanatoka gredi 6 kujiunga na shule hizo kote nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *