Ni rasmi sasa Alex Mwalimu ni mchezaji mpya wa klabu ya MOFA inayomilikiwa na mshambuliaji pamoja na nahodha wa timu ya taifa Michael Olunga.
Alex ametia saini mkataba wake mchana wa leo huko Homa Bay ambako ndio makazi ya klabu ya MOFA inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa.
Awali Alex alikuwa ameeleza matumaini yake kuwa atasheza katika kikosi cha timu ya taifa ya Harambe Stars kwani klabu ya MOFA inamfaa katika matayarisho ya safari ya soka hilo la kitaifa.
Alex Mwalimu maarufu kama Mbappe mzawa wa Matsangoni, 24, ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Young Bulls lakini pia SS Assad ya kwale inayoshiriki NSL.

