KUELEKEA msimu mpya wa CAF, Al Ahly imesalia kileleni mwa orodha ya Klabu bora bara Afrika, huku klabu ya SIMBA SC ikiwa klabu ya pekee Afrika Mashariki kutinga kwenye listi hiyo.
Kumeshuhudiwa ushindani mkubwa kwenye orodha hiyo, huku ES Tunis ya Tunisia ikipanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili, na kuipiku Klabu ya Rulani Mokwena, Wydad Athletic Club. Hii ni baada ya ES Tunis kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wydad, wakati huo huo, ilishuka hadi nafasi ya tatu baada ya kushindwa kutoka katika hatua ya makundi ya CAFCL musimu uliopita wa 2023/24, huku Sundowns ikisalia katika nafasi ya nne.
Kikosi kipya cha Mokwena kinatarajiwa kushuka zaidi katika orodha ya CAF kwani hawakufuzu kwa kampeni ya CAF ya 2024/25 kati ya vilabu, itakayoanza Ijumaa.
Wakati uo huo, vilabu kama Zamalek, RS Berkane, Simba SC, Petro de Luanda, TP Mazembe na klabu mpya ya Khanyisa Mayo, CR Belouizdad wanakamilisha 10 bora ya sasa.
10. CR Belouizdad (Algeria) – 36 points
9. TP Mazembe (DR Congo) – 38 points
8. Petro de Luanda (Angola) – 39 points
7. Simba (Tanzania) – 39 points
6. RS Berkane (Morocco) – 42 points
5. Zamalek (Egypt) – 48 points
4. Mamelodi Sundowns (South Africa) – 54 points
3. Wydad AC (Morocco) – 60 points
2. Esperance (Tunisia) – 61 points
1. Al Ahly (Egypt) – 87 points

