Rais William Ruto amemsuta aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagwa kutokana na kauli yake, ya misukosuko ya uongozi wa taifa hili, kwenye ziara yake kule Marekani.
Kulingana na Ruto, matamshi hayo hayakupaswa kutoka kwa kinywa cha kiongozi wa haiba yake, kwa kila anachosema amehudumu katika nafasi mbali mbali za uongozi kwenye serikali ya taifa hili kwa miaka mingi.
Rais Ruto ametilia shaka ombi la Gachagwa, kuwataka wakenya kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania urais wa taifa mwaka 2027, licha ya kuwa nchini ambayo limefeli katika utendakazi wake.
Wakati uo huo amewataka viongozi wote wa upinzani, wanaopinga uongozi wake kujitokeza na kuelezea wakenya, malengo na mipango walionayo katika kurekebisha makosa yanayo tekelezwa na serikali ya sasa.

