RIGATHI GACHAGWA AZIDISHA SHUTMA ZAKE DHIDI YA SERIKALI YA KITAIFA.

Kinara wa chama cha DCP, Geoffrey Rigathi Gachagwa, amesema mojawapo ya sababu zake kuondolewa kwenye nafasi ya naibu wa rais katika taifa hili, ni kutetea haki za wananchi wa kaunti ya Meru.

Akizungumza katika kaunti ya Meru, siku moja kabla ya rais William Ruto kufanya mkutano katika kaunti hiyo, Gachagwa amedai kuwa kulikuwa na njama, ya baadhi ya viongozi wa kuu katika eneo hilo kung’atuliwa kwenye nafasi zao za uongozi kitaifa.

Gachagwa ambaye amepigia debe chama chake katika eneo hilo, amedai kuwepo kwa njama za jamii ya eneo hilo, kugawanywa kwa misingi ya ukabila.

Aidha, amemsuta naibu wa rais Profesa Kithure Kindiki, kwa madai ya kutumika katika juhudi za kutatiza mikutano yake kaunti hiyo.