SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA YAKOSOLEWA KWA KUKATA MITI ILIYOKO KWENYE BUSTANI YA UHURU.

Maseneta wa kaunti ya Mombasa wamemsuta vikali gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassir, kwa kukata miti iliyodumu kwa miaka mingi katika bustani ya Uhuru kwenye jiji kuu ya Mombasa.

Wakiongozwa na seneta mteule Mirajj Abdulahi, wamesema kuwa zoezi hilo halikufuata sheria hitajika kwa mujibu wa katiba, hasa kipengele kinacho sisitiza haja ya wananchi kuhusishwa katika maamuzi yeyote ya serikali, hasa kuhusiana na mali ya umma.

Mirajj amepinga suala la miti hiyo kuwa na hatari kwa wananchi, akisema kuwa gavana Nassir, aliposwa kufanya zoezi hilo kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wa kaunti hiyo.

Kwa upande wake seneta Mohammed Faki, amesema kuwa miti hiyo ilikuwa ikisaidia pakubwa kusafisha hewa chafu, inayotoka kwa viwanda na kuchafua mazingira ya eneo hilo na kuongeza kuwa gavana huyo, alipaswa kukata matawi na wala sio miti yenyewe.