Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagwa, amewasuta vikali baadhi ya wabunge wa eneo Mlima Kenya, kwa kuendelea kumuunga mkono rais William Ruto.
Kulingana na Gachagwa, viongozi wanaounga mkono Serikali kuu, waendelea kupotosha wananchi katika eneo hilo, kwani huenda wakakosa kunufaika na matunda ya uongozi wa rais Ruto.
Akizungumza katika eneo bunge la Lari kaunti ya Kiambu, Gachagwa amedai kuwa baadhi ya viongozi hao, wamekuwa wakitumika zua Rapsha kwenye mikutano yake.
Aidha, kiongozi huyo aliyekuwa naibu wa rais katika taifa hili, ameibua madai ya rais William Ruto kunuafisha jamii yake pekee na kutumia vibaya vijana katika eneo la Mlima Kenya.

