Serikali ya kitaifa imesema itaanzisha mpango wa wakenya wamapato ya chini, kumudu gharama ya malipo ya bima mpya ya afya SHA.
Kulingana na rais William Ruto, mpango huo utasaidia pakubwa wakenya kupata huduma za afya, katika hospitali yeyote ndani ya taifa hili.
Akizungumza katika kaunti ya Homa Bay, kwenye maadhimisho ya siku ya Madakaraka, kiongozi wa taifa amesema kuwa serikali kuu, inajitahidi kuboresha shughuli za afya nchini.
Aidha, Rais Ruto amepigia debe mfumo wa SHA, akisema kuwa umesaidia pakubwa wakenya hasa wa mapato ya chini, kupata huduma za afya za dharura ,wakati wanapo ugua.

