WAKAAZI WA KAUNTI YA HOMA BAYA WASISITIZWA KUUNGA MKONO SERIKALI YA MUUNGANO.

Rais William Ruto amewataka wakenya katika kaunti ya Homa Bay kuunga mkono na serikali yake, ili kushuhudia maendeleo katika eneo hilo.

Akihutubia wananchi, Ruto amewaonya dhidi ya kukubaliana na kauli za wapinzani wake, wanao ongozwa na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagwa.

Rais amekashifu viongozi wa upinzani, akidai wamekuwa wakiendeleza fitina dhidi ya serikali yake, huku akiongeza kuwa hawana mpango wowote wa kuboresha maisha ya wakenya.

Kwa upande wake Raila Odinga aliyekuwa waziri mkuu na mpinzani mkubwa wa rais amewahakikishia wananchi wa kaunti hiyo kuwa kamwe, hata ungana na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, kwa madai kuwa kiongozi huyo wa upinzani, amekuwa akiendeleza siasa zinazo weza kuchangia migawanyiko kati ya wakenya.