Mwanasheria mkuu nchini Dorcas Odwor amepinga madai ya kuhamishwa kwa muhuri maalum wa serikali kuu kutoka kwa afisi yake na kupelekwa katika afisi ya mkuu wa watumishi wa umma nchini Felix Koskei.
Odwor ameweka wazi kuwa muhuri huo, ungali unadhibitiwa na afisi yake kwa mujibu wa sheria za taifa hili.
Akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa sheria hiyo bado haija badilishwa wala kukiukwa na badala yake inatiliwa maanani kiukamilifu na afisi yake.
Aidha, amewataka wakenya kupuuza masuala ambayo wamekuwa wakisikia kuhusiana na suala la kuhamishwa kwa muhuri wa serikali kuu na kuongeza kuwa afisi yake, inashirikiana na ile ya mkuu wa watumishi wa umma, ili kufanikisha majukumu yao.

