RAIS WILLIAM RUTO ANGALI KUSIFIA MUUNGANO WAKE NA RAILA ODINGA.

Rais William Ruto amewakashifu pakubwa baadhi ya wapinzani wake, ambao wameendelea kupinga miradi ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Akizungumza katika ziara yake kule kaunti ya Kisumu, rais Ruto amempongeza aliyekuwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga, kwa kumsaidia katika kuboresha maendeleo ya taifa hasa katika eneo hilo.

Rais amewataka wapinzani wake kuto ingiliakati umoja wa serikali yake na viongozi waliokuwa mrengo wa upinzani na badala yake kuwapa mda wa kufanya maendeleo.

Kiongozi wa taifa amezungumza hayo baada ya kuweka jiwe la msingi, katika mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kaunti ya Kisumu.

Kwa upande wake Raila Odinga, ameunga mkono mradi huo wa serikali ya kitaifa, kwa kile alichosema una uuwiana na sheria za taifa hili.