Kaunti ya Taita Taveta imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya hedhi duniani.
Waziri wa jinsia katika kaunti hiyo Shedrak Mutungi amesema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi katika kaunti hiyo, wameendelea kupitia changamoto ya ukosefu wa sodo katika siku zao za hedhi.
Waziri Mutungi, ameelezea kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakikosa kuhudhuria masomo shuleni, kufuatia hatua yao kukosa sodo wakati wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
Ni hatua ambayo imechangia pakubwa kudorora kwa viwango vya elimu kwa baadhi ya wanafunzi wa kike katika maeneo ya mashinani kaunti hiyo.
Aidha, amepongeza wadau ambao wamejitokeza kuendeleza ugavi wa soko kwa wanafunzi wa shule za Marasi iliyoko katika kaunti hiyo ya Taita Taveta.

