Wanawake kaunti ya Mombasa wamewaonya dhidi ya kuvumilia dhulma wanazofanyiwa na waume zao kwenye ndoa.
Kulingana na mwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa Zamzam Mohamed, akina mama wanapaswa kujitokeza na kuripoti visa vya dhulma za kijinsia, vinavyo tekelezwa dhidi yao, ili hatua za kisheria zichukuliwe na wanahusika waadhibiwe.
Akizungumza katika kaunti hiyo, mwakilishi huyo wa kike vile vile, amekashifu vikali visa vya dhulma za kingono, ambazo katika siku za hivi majuzi, zimekuwa zikifanyiwa watoto wadogo kwenye jamii.
Aidha, amesema kuwa kuna haja ya kupitishwa kwa sheria ya wanaume wanaotekeleza visa hivyo kuwakata sehemu za siri wanapo patikana na hatia ya kulawiti ama hata kubaka watoto wadogo.
Kwa upande wake mbunge wa Kisauni kaunti ya Mombasa, Rashid Bedzimba amewaonya wanawake dhidi ya kukubaliana na baadhi ya vishawishi wanavyopewa na wanaume kwenye jamii.

