Mkuu wa mawaziri ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi, amewaonya wanasiasa dhidi ya kuchochea machafuko kwenye uchaguzi wa mwaka 2027.
Kulingana na Mudavadi, hakuna kiongozi wa kisiasa ambaye anapaswa kukumbusha wakenya matukio hayo, kwani anawatia hofu ya kushiriki uchaguzi huo mkuu.
Akizungumza katika eneo la Malava kaunti ya Kakamega, Mudavadi amesema kuwa kufikia sasa, Kenya imepiga hatua kubwa katika masuala ya usalama na umoja, hasa wakati kunapokuwa na uchaguzi na kwemwe matukio hayo hayapaswi kurejelewa tena.
Waziri huyo wa mambo ya inje, amemsuta aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, kwa madai ya kuendeleza vitisho kwa wakenya.

