Ukosefu wa fedha za kutosha kwenye bajeti ya kila mwaka ya serikali ya kaunti ya Kwale, ndiyo chanzo cha serikali hiyo kushindwa kufanikisha ujenzi wa maeneo ya kuhifadhi waathiriwa wa dhulma za kijinsia.
Haya ni kulingana na waziri wa masuala ya jamii na talanta kaunti hiyo Francisca Kilonzo, hifadhi hizo ni paswa kujengwa katika eneo bunge la Lunga Lunga na Kinago, sehemu ambazo anasema zimeripoti visa vingi vya dhumla za kijinsia.
Waziri Kilonzo amewataka wananchi katika maeneo bunge hayo, kujitokeza kwenye vikao vya umma vinavyo endeshwa ili kuwapatia fursa ya kupendekeza miradi wanayotaka kufanyiwa na serikali ya kaunti ya Kwale.
Mwanachama wa jopo kazi la dhulma na mauaji ya wanawake Mohammed Washala amesema kuwa taifa hili limeshuhudia ongezeko la asilimia nane ya visa vya mauaji ya wanawake mwaka huu wa 2025.

