RAIS WILLIAM RUTO ASIFIA NDOA YAKE NA RAILA ODINGA.

Rais William Ruto amewaonya viongozi katika nafasi mbali mbali kwenye serikali yake, dhidi ya kuendeleza siasa na badala yake kufanya maendeleo.

Kulingana Rais, kwa sasa ni wakati wa wananchi kufaidi matunda ya uchaguzi, kupitia kufanikishwa kwa miradi ya maendeleo mashinani.

Akizungumza katika ziara yake kule kaunti ya Narok, rais amesisitiza haja ya wakenya, kuungana na kuweka kando tofauti za kisiasa, ili kuboresha masuala ya maendeleo.

Na kama ilivyo ada yake, rais hajakosa kupigia upatu muungano kati yake na aliyekuwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga, akisema kuwa umoja wao, ni mojawapo ya hatua muhimu katika kufanikisha maendeleo ya jamii.