Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Meru, Kawira Mwangaza amesema kuwa atazindua chama chake kitakacho mpatia fursa ya kuwania ugavana wa kaunti hiyo kwa mara nyingine.
Kawira ambaye alibanduliwa mamlakani na bunge la kaunti ya Meru, amesema kuwa hatua yake kuwa mgombea huru, ni mojawapo sababu zake kukosa kupata utetezi dhidi ya mswada wa kumuondoa mamlakani kwenye bunge hilo.
Katika taarifa yake kwa wanahabari, Kawira amesema licha ya chama hicho kuwa na viongozi wengi wa kaunti ya Meru, pia kitajumuisha viongozi wengine katika kaunti tofauti za taifa hili.
Aidha, ameelezea kuwa kwa sasa wanafanya mazungumzo na wananchi katika kaunti hiyo, ili kusikiliza maoni yao kuhusiana na suala hilo.

